
Aliyekuwa Rasi wa pili wa Zambia, Frederick Jacob Titus Chiluba (68), amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo nchini Zambia. Chiluba, ambaye aliiongoza Zambia kuanzia mwaka 1991 - 2002, hadi jana mchana inadaiwa alionekana mwenye afya njema, lakini ilipofika saa 6 usiku aliugua ghafla na kuaga duania. Hadi sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu sababu za kifo chake.
No comments:
Post a Comment