Monday, April 11, 2011

Uzinduzi wa Miriam lukindo...




UZINDUZI wa albamu ya video ya ‘Ni Asubuhi’ ya mwanamuziki nyota wa Injili, Miriam Lukindo, akishirikiana na Haak Neel Production, uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam wikiendi hii, ulifana kwa hali ya juu baada ya kuvutia mamia ya mashabiki. 
Uzinduzi huo uliowakutanisha waimbaji maarufu wa Injili wakiwemo Upendo Nkone, Maron Shako kutoka Kenya na Martha Mwaipaja na kwaya mbalimbali maarufu nchini, uliwafanya watu waliohudhuria katika hafla hiyo kuacha viti vyao na kujikuta wakiimba na kuserebuka kwa pamoja na waimbaji hao.






No comments:

Post a Comment