Saturday, April 9, 2011

Wayne Rooney na kashfa ya Maneno machafu...






LONDON, England
RUFAA ya mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney kutaka asiadhibiwe kukosa mechi mbili baada ya kutoa lugha chafu mbele ya kamera wiki iliyopita, alipokuwa akishangilia bao katika mechi dhidi ya West Ham imekataliwa.

Taarifa ya Chama cha Soka cha England (FA) iliyotolewa jana jioni imeeleza Rooney atakosa mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Fulham wikiendi hii na ina ile ya Manchester City katika nusu fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Wembley wiki ijayo.

Rooney kupitia msemaji wake Ian Monk amesema: “Mimi siyo mchezaji wa kwanza kushangilia mbele ya kamera ya televisheni na sitakuwa wa mwisho. Wengi wanafanya hivyo, hii si haki.”

No comments:

Post a Comment