Friday, April 8, 2011

Hii tena funga kazi....

MSHINDI  wa  taji la  Miss  Ilala  2008, Sylvia Shally  anataka  kuzaa watoto kumi pindi atakapojaaliwa kupata mume wa  kumuoa,  Ijumaa  limeinyaka.  

Akizungumza  kwenye mahojiano maalum na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki kwenye Mgahawa wa Stears Kijitonyama jijini Dar, Shally alisema kuzaa watoto kumi ndiyo ndoto aliyonayo ambayo amepanga kuitimiza atakapoolewa.   

“Katika maisha kila mtu ana jambo ambalo anaamini  litampa faraja kubwa, haijalishi kama itakuwa au la, ndoto yangu ni kuzaa watoto kumi pindi nitakapoolewa, namuomba Mungu anipatie mume mwema mwenye kuelewa mambo ili niweze kutimiza ndoto hiyo,” alisema Shally.

Akiendelea zaidi Shally aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na mcheza filamu maarufu nchini, Steven Kanumba, alisema anajua watu wanaweza  kumshangaa kwa kauli yake hiyo kutokana na hali halisi ya maisha ya sasa lakini hilo halitamfanya aipotezee ndoto hiyo.

No comments:

Post a Comment